Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 12:18-26 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.

19. Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20. Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.

21. Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: “Sikuhitaji wewe,” wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: “Siwahitaji nyinyi.”

22. Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.

23. Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,

24. ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima,

25. ili kusiweko na utengano katika mwili, bali viungo vyote vishughulikiane.

26. Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 12