Agano la Kale

Agano Jipya

1 Petro 5:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao.

7. Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

8. Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo.

9. Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.

10. Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.

11. Kwake yawe mamlaka milele! Amina.

Kusoma sura kamili 1 Petro 5