Agano la Kale

Agano Jipya

1 Petro 3:10-21 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Anayetaka kufurahia maisha,na kuona siku za fanaka,ajizuie asiseme mabayaaepe kusema uongo.

11. Ajiepushe na uovu, atende mema,atafute amani na kuizingatia.

12. Maana Bwana huwatazama kwa wema waadilifuna kuzisikiliza sala zao.Lakini huwapa kisogo watu watendao maovu.”

13. Ni nani atakayeweza kuwadhuru nyinyi kama mkizingatia kutenda mema?

14. Lakini, hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, basi, mna heri. Msimwogope mtu yeyote, wala msikubali kutiwa katika wasiwasi.

15. Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,

16. lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema, kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema kama Wakristo, waone aibu.

17. Maana ni afadhali kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, kama Mungu akipenda, kuliko kuteseka kwa sababu ya kutenda uovu.

18. Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;

19. na kwa maisha yake ya kiroho alikwenda kuwahubiria wale roho waliokuwa kifungoni.

20. Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,

21. ambayo yalikuwa mfano wa ubatizo unaowaokoa nyinyi sasa. Ubatizo si shauri la kuondoa uchafu mwilini, bali ni ahadi kwa Mungu inayofanyika katika dhamiri njema. Huwaokoeni kwa njia ya ufufuo wa Yesu Kristo

Kusoma sura kamili 1 Petro 3