1. Hapo Yobu akajibu:
2. “Mambo kama hayo nimeyasikia mengi;nyinyi ni wafariji duni kabisa!
3. Mwisho wa maneno haya matupu ni lini?Au ni kitu gani kinachowachochea kujibu?
4. Kama nyinyi mngekuwa mimi, na mimi nyinyi,ningeweza kusema kama nyinyiningeweza kubuni maneno dhidi yenu,na kutikisa kichwa changu.
5. Ningeweza kuwatia moyo kwa maneno yangu,na maneno yangu ya faraja yangewatuliza.