16. Mataifa hayo yatakunywa na kupepesuka na kurukwa na akili kwa sababu ya mauaji nitakayosababisha kati yao.”
17. Basi, nikachukua hicho kikombe mkononi mwa Mwenyezi-Mungu, nikayanywesha mataifa yote ambayo Mwenyezi-Mungu alinituma kwao.
18. Kwanza Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na viongozi wake, ili kuifanya iwe jangwa, ukiwa, kitu cha kuzomewa na kulaaniwa, kama ilivyo mpaka leo. Halafu:
19. Farao, mfalme wa Misri, maofisa na viongozi wake, pamoja na watu wake wote;
20. wageni wote walioishi nchini Misri; wafalme wote wa nchi ya Uzi; wafalme wote wa miji ya Wafilisti, Ashkeloni, Gaza, Ekroni na mabaki ya Ashdodi.
21. Watu wote wa Edomu, Moabu na Amoni;
22. wafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ya bahari ya Mediteranea;
23. wakazi wa Dedani, Tema, Buzi na watu wote wanyoao denge;
24. wafalme wote wa Arabia; wafalme wote wa makabila yaliyochanganyika jangwani;