30. Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga,na kuwa tayari kupokea matusi yake.
31. Mwenyezi-Mungu hatatutupa milele.
32. Ingawa atufanya tuhuzunike,atakuwa na huruma tenakadiri ya wingi wa fadhili zake.
33. Yeye hapendelei kuwatesawala kuwahuzunisha wanadamu.
34. Wafungwa wote nchiniwanapodhulumiwa na kupondwa;
35. haki za binadamu zinapopotoshwambele yake Mungu Mkuu,
36. kesi ya mtu inapopotoshwa mahakamani,je, Mwenyezi-Mungu haoni hayo?