Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba.Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena,wala kupiga vigelegele.Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni,sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.