7. Idadi yao pamoja na wale ndugu zao Walawi waliofundishwa kumwimbia Mwenyezi-Mungu, wote waliokuwa stadi, ilikuwa 288.
8. Wote, wakubwa kwa wadogo, waalimu kwa wanafunzi, walitumia kura katika kupanga kazi zao.
9. Kura ya 1 ilimwangukia Yosefu wa jamaa ya Asafu; ya 2 Gedalia pamoja na ndugu zake na wanawe kumi na wawili;
10. ya 3 Zakuri pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili;
11. ya 4 ilimwangukia Seri pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili;
12. ya 5 Nethania; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili;
13. ya 6 Bukia; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili;
14. ya 7 Asharela; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili;